Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imepokea viti 80 na kompyuta 15 toka kwa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) ambapo viti hivyo na kompyuta hizo zitaelekezwa katika ofisi mbalimbali kwa matumizi ya ofisi.
Zoezi la upokeaji vifaa hivi limefanyika leo Novemba 14, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, ambapo viti vyote 80 vimeshapokelewa na kesho saa 7 mchana, kompyuta 15 zitpokelewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Dkt. Omary A. Nkullo anatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Benki ya NBC na pia kuziomba benki zingi kutoa misaada kwa taasisi mbalimbali katika masuala ya maendeleo ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.