Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Mayeka Simon Mayeka amemuagiza Afisa maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwakamata wanavikundi wote waliokaidi kulipa marejesho na wanadaiwa mkopo wa asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mhe Mayeka ameyasema hayo katika kikao kilichoandaliwa na Idara ya maendeleo ya jamii ili kuona namna gani wanaweza kuweka mikakati itakayosaidia kurejeshwa kwa fedha zinazodaiwa na vikundi 84 kiasi cha shilingi 359,593,912.5 ambazo hazijalipwa.
"suala la ukamataji ni la lazima wakamatwe wanavikundi wote waliokaidi kulipa, tushirikiane sababu hili jambo ni letu sote" amesema Mhe. Mayeka.
Awali akiwasilisha taarifa ya mikopo ya 10% kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Afisa maendeleo ya jamii ndugu Alphonce Mkwizu amesema kuwa Awali Deni lilikuwa 498,448,750 lakini baada ya kuweka kikosi kazi cha kukamata na kuvifikisha mahakamani vikundi vinavyodaiwa walifanikiwa kurejesha zaidi ya milioni 138 sawa na 28% ya fedha zilizokuwa zikidaiwa.
Aidha Ndg Mkwizu ameongeza kuwa urejeshaji wa fedha hizo umekuwa mgumu kutokana na vikundi kupuuzia madeni, kufeli kwa Miradi ya vikundi, kutoaminiana kwa viongozi wa vikundi, ushirikiano mdogo wa Watendaji Kata katika kufatilia madeni na changamoto ya ukosefu wa usafiri kufatilia madeni kwa vikundi hivyo.
Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bwana Fortunatus Mabula amesema kuwa licha ya ugumu wa kazi hiyo lakini Watendaji wa Kata wasimamie zoezi la upatikanaji wa fedha hizo kwa niaba ya Mkurugenzi kwani kupatikana kwa fedha hizi kutasaidia vikundi vingine kupata fursa hiyo ya fedha siku za usoni.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.