DC KONGWA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA AKIBA 2025
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari- Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Mayeka Simon Mayeka amefunga rasmi mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba Wilaya ya Kongwa 2025 ambapo askari 52 wamehitimu mafunzo hayo.
Wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kata ya Chamkoroma Kijiji cha Tubugwe juu Mh Mayeka amewataka wahitimu kutambua jukumu lao kubwa zaidi la kuipambania Nchi, kuihudumia jamii na kushirikiana na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.
Aidha Mh Mayeka ametumia wasaa huo kuongea na Wananchi kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kutunza amani katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Kwa upande wake Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Kongwa Meja Joseph Mwandemo ametoa wito kwa wahitimu hao kutunza nidhamu ya mafunzo waliyopewa ndani ya nchi.
Akiongea kwa niaba ya wahitimu wengine Mgm Chensia Laurent ameishukuru Serikali kwa kuanzisha mafunzo hayo na kuwashukuru wakufunzi wa mafunzo kwani yamewasaidia kuelewa umuhimu wa Askari na wajibu wao katika kulinda Nchi wakati wote.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.