Na Stephen Jackson, Kongwa DCM
kuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, amewataka wafanya biashara wa Sukari kuuza bidhaa hiyo kwa kuzingatia bei elekezi ya serikali ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama za bidhaa hiyo inayodaiwa kuadimika. "Toeni sukari kama ipo uzeni hata kama ni kwa faida ndogo, wapeni wananchi wanywe chai"
Mhe. Mayeja alitoa agizo hilo Januari 31, 2024, kwa wafanyabiashara wenye maduka yanayouza sukari jumla na rejareja Wilayani Kongwa, alipoitisha kikao maalumu kufuatia dalili za kuadimika kwa sukari kulikopelekea baadhi ya wafanya biashara kutozingatia bei elekezi ya serikali huku wengine wakificha bidhaa hiyo na kupelekea usumbufu kwa wananchi. "Juzi nilimtuma dereva wangu dukani akaninunulie sukari. Hadi mimi mwenyewe nimekosa sukari" alinukuliwa Mayeka.
Yote hayo yamejiri kufuatia mazungumzo baina yao na Kamati ya usalama ya Wilaya na Maafisa biashara wa Halmashauri kupitia kikao maalumu kilichoitishwa na mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka Januari 31, 2024 ofisini kwake.
Wakitoa michango yao baadhi ya Wafanya biashara walisema, bei elekezi iliyotolewa na Serikali hivi karibuni imewaathri baadhi ya wafanya biashara wa Jumla na rejareja kwani tayari walikuwa wameshanunua sukari hiyo kwa bei ya juu hivyo kuna uwezekano wa kuficha sukari kutokana na kushindwa kuuza kwa bei elekezi agizo, linalodaiwa kuwapa hasara.
Priscus Shirima mfanyabiashara mashughuli Mjini Kongwa, alisema upo uhaba wa sukari nchini kutokana na viwanda vya ndani kupunguza uzalishaji kipindi cha masika hivyo ameiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa sukari nchini hasa kwa kipindi cha masika ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Afisa biashara Wilaya ya Kongwa Bwana Yonaza Mchome alisema, ni wajibu wa wafanyaniashara kuzingatia bei elekezi na si vinginevyo kwani ofisi ya biashara itafanya msako mkali katika maduka na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuuza sukari nje ya bei elekezi.
Hata hivyo kupitia kikao hicho, Jeshi la Polisi Kongwa limeahidi kushirikiana na wataalamu wa biashara na wadau wengine kufanya msako mkali katika maduka ili kuwabaini wafanya biashara wanaoficha sukari kwa lengo la kuuza kinyemela na kuwachukulia hatua za kisheria.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.