DC MAYEKA AFANYA UKAGUZI WA UJENZI WA JENGO LA WODI YA WAZAZI NA UPASUAJI
Mh. Mayeka S Mayeka amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi na upasuaji katika kituo cha afya Lenjulu na baada ya kusomewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, Mh. Mayeka ameelekeza kamati ya ujenzi pamoja na viongozi wa Serikali kufuatilia hati ya eneo linalofanyika ujenzi pamoja na kuandaa na kutunza nakala za mapokezi ya vifaa vya ujenzi ili kuwe na kumbukumbu ya maandishi.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Mayeka S Mayeka akikagua tofali zinazotumika katika ujenzi wa jengo hilo
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo ameeleza kuwa ujenzi wa jengo hilo la wazazi na upasuaji unatekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri, ambapo hadi sasa Halmashauri imetoa kiasi cha Tsh. 85,496,740/= ambazo zimetumika kwa malipo ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi, malipo ya mafundi na gharama nyingine.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.