Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka amefunga mafunzo ya kujengewa uwezo wa kufanya Tathmini kwa kutumia Mfumo wa Uthibiti Ubora wa Shule (School Quality Assurance System - SQAS) kwa maafisa elimu Kata, walimu wakuu na wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na wenyeviti wa kamati za uthibiti ubora wa shule wa ndani ya Wilaya.
Mhe Mayeka ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa zinazofanywa katika kuboresha Sekta ya Elimu.
Mhe. Mayeka amegusia umuhimu wa mafunzo hayo kwa kueleza kuwa yanasaidia kuboresha utendaji kazi wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule kwa kufanya tathmni kidigitali hatua kubwa iliyofikiwa kwani hapo awali tathmini zote zilifanyika kwa kutumia makaratasi na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yanaenda kuboresha ufanyaji tathmini kuanzia ngazi za Shule hadi Halmashauri.
katika mafunzo hayo washiriki wamejifunza ujazaji wa Fomu za School Self Evaluation Form (SSEF) ambazo zinasaidia shule kujitathmini yenyewe kwa kujipima na kuona namna inavyotekeleza majukumu yake ya kila siku.
jumla ya washiriki 370 wamepatiwa mafunzo katika Vituo vinne (04) kwa shule za Binafsi na Serikali ambapo Msingi washiriki 130 na Sekondari washiriki 44. Aidha, jumla ya Maafisa Elimu Kata 22, Walimu Wakuu 130, Wakuu wa Shule 44 na Wenyeviti wa Kamati za Uthibiti Ubora wa Shule wa Ndani 174 wamepatiwa Mafunzo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.