Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka amewataka wananchi kushiriki kwenye shughuli za utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na usafi wa kila jumamosi na upandaji miti katika maeneo yao.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti lililofanyika Januari 16, 2024 Mhe. Mayeka amezielekeza taasisi mbalimbali Wilayani Kongwa kuwa na mipango ya muda mrefu ya matumizi ya ardhi, itakayowezesha taasisi hizo kutunza miti inayopandwa katika maeneo hayo.
Akizungumzia kampeni ya usafi kwa siku za Jumamosi, amesema Wilayani kongwa kwa sasa usafi unafanyika Kila Jumamosi badala ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kama ilivyopangwa kitaifa.
Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa taratibu, Wananchi waliopakana na barabara wanawajibika kusafisha hadi barabarani na pia katika siku za usafi wa Mazingira wafanya biashara hawana sababu ya kufunga maeneo yao ya biashara kwani kinachotakiwa ni kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa katika hali ya usafi. "Kwa kuona umuhimu, kuna siku atafunga duka yeye mwenyewe ili akafanye usafi" Mhe. Mayeka.
Kupitia hafla hiyo Mayeka ametoa wito kwa jamii na taasisi za umma kuachana na mazoea ya kupanda miti mingi kwa pamoja pasi na mikakati thabiti ya kuitunza., hukuakipiga marufuku ukataji holela wa miti pasipokuwa na vibali. " Vibali vya kukata miti vinatolewa na Ofisi ya mkuu wa Wilaya au kwa Watendaji wa kata kwa niaba." Alisema Mayeka.
Katika Mazungumzo yake Mhe. Mayeka alizitaka taasisi zote za umma kutekeleza agizo la upandaji miti kama ilivyoazimiwa ili wananchi waweze kuhamasika na kuunga mkono jitihada za serikali katika uhifadhi wa mazingira.
Naye Dkt. Omary A. Nkullo Mkurugenzi Mtendaji (W) alisema Halmashauri imekusudia kupanda miti kwenye eneo lote la Hospitali ya Wilaya lenye ukubwa wa ekari 21, kwa kuwa ipo miche ya kutosha ambapo zaidi ya miti 200 imepandwa katika hafla hiyo.
Akizungumza kikao hicho, afisa Maliasili na mazingira bwana Godfrey Mujairi alitaja shughuli za kibinadamu kama changamoto kubwa inayopelekea uharibifu wa Mazingira ikiwemo uvamizi wa misitu na maeneo ya uchimbaji madini, ukataji miti ovyo, kilimo na ufugaji holela na utupaji hovyo taka kando ya barabara.
Zoezi la upandaji miti limehusisha kamati ya usalama ya Wilaya, Wakuu wa Divisheni naVitengo, wananchi na watumishi ambapo Mhe. Mayeka alipanda mti kama ishara ya uzinduzi wa zoezi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.