Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Mayeka Simon Mayeka amekabidhi misaada mbalimbali yakiwemo magodoro kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Akiongea wakati akikabidhi misaada hiyo ofisini kwake, Mhe. Mayeka Simon Mayeka amesema kuwa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Kongwa anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuona umuhimu wa kusaidia makundi ya watoto wenye uhitaji waliopo katika Wilaya ya Kongwa.
Licha ya kusisitiza matunzo lakini pia Mhe. Mayeka ameeleza kuwa kuna Wilaya na shule nyingi Tanzania lakini Kongwa imekuwa ni sehemu ya waliopewa misaada hiyo hivyo anaamini misaada hiyo itawafikia walengwa kama ilivyoelekezwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. White Zuberi amepongeza na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitaleta manufaa na tija kwa wanafunzi hao na vitatosha kwa wanafunzi wote waliokusudiwa na kuitaka jamii kuiga mfano wa Mhe. Rais wa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amezitaja shule zenye vituo vya wanafunzi wenye ulemavu zilizopata misaada hiyo kuwa ni Pamoja na shule ya msingi mkoka yenye wanafunzi 122, shule ya msingi Kongwa mjini yenye wanafunzi 34 na shule ya msingi Mlali B yenye wanafunzi 56.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.