Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Mayeka Simon Mayeka ametembelea Kata ya Makawa iliyoko wilayani Kongwa na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Muungano, ujenzi wa kliniki ya baba, mama na mtoto katika kijiji cha Makawa na kufanya mkutano wa hadhara kuongea na Wananchi wa Kata hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe Mayeka licha ya kupongeza wananchi wa Kata hiyo kwa hatua ya kuanzisha shughuli za miradi ya maendeleo katika Maeneo yao lakini pia ameshukuru shirika lisilokuwa la kiserikali la World Vision kwa ujenzi wa kliniki ya baba, mama na mtoto ambayo imegarimu shilingi milioni 42,742,750 mpaka sasa ambapo ujenzi umefikia katika hatua ya umaliziaji.
Aidha Mhe Mayeka ameagiza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kusaidia hatua ya umaliziaji wa Zahanati hizo kwa haraka ili kutatua changamoto ya miundombinu ya afya katika Kata hiyo na pia kuwatia moyo na kuwaunga mkono wananchi kwa juhudi walizozionyesha.
"Safari ya maendeleo ni hatua huwezi kumaliza Kila jambo Kwa wakati mmoja, najua mna mambo mengi mnayohitaji; niwahakikishieni jukumu letu viongozi kuja kusikiliza kero zenu na kutolea majawabu" alisema Mayeka.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.