Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka ameagiza uongozi wa Halmashauri kufanya maboresho katika soko la mazao Kibaigwa ili liweze kuongeza mapato ya Halmashauri.
Mhe. Mayeka alitoa maelekezo hayo katika kikao maalumu kilichohusisha kamati ya usalama (W) pamoja na uongozi wa soko hilo Aprili 23, 2024 alipofanya ziara ya kuona hali ya uendeshwaji wa Soko.
Akiwasilisha taarifa ya soko, kaimu meneja wa Soko hilo Emmanuel Kereyani alisema kwa mwaka wa fedha 2023/24 soko hilo lilitarajiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni moja na hadi sasa makusanyo yamefikia 68% ya fedha hizo.
Kupitia ziara hiyo ya siku moja, Mhe. Mayeka alikagua sehemu ya eneo na shughuli za soko na utaratibu mzima wa uendeshwaji, ambapo alielekeza Halmashauri kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha soko hilo linazingatia vigezo vya ushindani ikiwa ni pamoja na kuhakikisha changamoto mbalimbali zinashughulikiwa kikamilifu.
Ziara hiyo ya Kamati ya usalama iliyofanyika Soko la mazao Kibaigwa ilihusisha baadhi ya wataalamu kutoka Halmashauri na uongozi wa Mamlaka ya mji mdogo Kibaigwa
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.