NA. Bernadetha S Mwakilabi
Habari- Kongwa DC
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amewataka wakuu wa idara na vitengo kuwafanyia tathmini watumishi walio chini yao ili wasiwe vikwanzo kwa watumishi hao kupata stahiki zao kama kupandishwa vyeo.
Dkt. Omary ameeleza hayo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya e_utendaji kwa watumishi wa umma yaliyofanyika Wilayani Kongwa ambapo amewataka watumishi hao kuelewa na kuyachukulia uzito mafunzo hayo ili waweze kuwasimamia vizuri watumishi walio chini yao.
Kwa upande wake Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya kongwa Bw. Fortunatus Mabula ameeleza kuwa mafunzo haya yamekuja baada ya kuonekana kuwepo kwa changamoto za mipango ya utendaji kazi inayoandaliwa kutopimika kwa wakati.
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Utumishi makao makuu Bw. Josephat Manyama amefafanua kuwa Ofisi ya Rais imeona kuna haja ya kuwajengea uwezo watumishi na viongozi kwa kuwapitisha katika mafunzo hayo ya mfumo kwani mwaka uliopita wasimamizi hawakufanya vizuri katika kufanya tathmini na kupelekea watumishi kukosa stahiki zao.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.