Halmashauri ya wilaya ya Kongwa imekabidhi pikipiki tatu kwa watendaji wa Kata za Chiwe, Zoissa na Ngomai zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuboresha na kurahisisha kazi za Watendaji wa Kata.
Akikabidhi pikipiki hizo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa Bwana Fortunatus Mabula amepongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwawezesha watumishi hao kwa kuwapatia usafiri utakaowasogeza karibu zaidi na wananchi.
Aidha Bwana Fortunatus Mabula amewasisitiza watendaji hao kutunza pikipiki hizo na kuzingatia matumizi sahihi ya pikipiki hizo ili kurahisisha kazi za serikali na kufikia wananchi wa sehemu husika.
Akiongea kwa niaba ya Watendaji wa Kata waliokabidhiwa pikipiki hizo Mtendaji wa Kata ya Ngomai Bwana Anord Sewando ametoa shukrani kwa Serikali kwa kuona umuhimu wa kazi zao kwani Watendaji wa kata ni kiunganishi muhimu kati ya serikali na wananchi.
Hii ni awamu ya pili ya makabidhiano ya pikipiki kwa Watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.