Na Stephen Jackson, Kongwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Imekabidhi vyumba 130 vya Madarasa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel leo Tarehe 31 Disemba 2021.
Akiwasilisha taarifa ya Makabidhiano, Mkurugenzi Mtendaji (W) Dr. Omary Nkullo, ameeleza changamoto walizokabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa mradi ikiwemo mfumuko wa bei ya vifaa vya ujenzi, Ukosefu wa maji kwa badhi ya Maeneo, baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kuchangia nguvu kazi, na kukatika kwa umeme mara kwa mara
Miongoni Mwa Madarasa yaliyokabidhiwa, kumi na nane (18) ni madarasa ya shule shikizi za msingi, na Miamoja kumi na mbili ni (112) ni shule za Sekondari.
Akihutubia wananchi wa kata ya Ugogoni, Mkuu wa Wilaya Mhe. Remidius Emmanuel, amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Kwanza kuripoti mapema pindi shule zitakapofunguliwa, kwa kuwa kwa sasa hakuna kisingizio.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ugogoni Mhe. Elizabeth Lenjima, ameishukuru serikali kwa kusaidia kuondoa kero ya wanafunzi kubanana Madarasani, jambo litakalosaidia kwenye mapambano dhidi ya Virusi vya "Corona"
Makabidhiano hayo yamefanyika kiwilaya katika shule ya Sekondari Ibwaga mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, viongozi mbalimbali kutokahalmashauri pamojana wananchi. Baada ya hafla hiyo Viongozi hao waliendelea na ziara kutembelea baadhi ya madarasa hayo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.