Halmashauri ya Wilaya Kongwa yatunukiwa cheti cha wateja bora kwa mwaka 2017 na Benki ya NMB Tawi la Kongwa. Cheti hicho kimekabidhiwa siku ya tarehe 5 Februari, 2018 katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kongwa Bwana Tuntufye Jacob Mwakatika ameeleza kwamaba "Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ni mteja bora kabisa kati ya wateja waliosaidia kuvuka malengo ya mwaka 2017. Hivyo, katika kutambua mchango wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa, Benki yetu, imeamua kutoa cheti cha wateja bora kwa mwaka 2017". Haya ameyasema wakati akikabidhi cheti hicho kwa Mkuruguenzi Mtendaji Eng. Ngusa L. Izengo tukio likishuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmshauri Mhe White Zuberi Mwanzalila, na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA (W) Bwana Nkinde Moses.
Fungua kiungo hapa chini kuona cheti kilichokabidhiwa.
Cheti cha Wateja Bora kwa Mwaka 2017 kwa Benki ya NMB Tawi la Kongwa..pdf
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.