Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imegawa jumla ya lita 446 za maziwa sawa na pakiti 1783 zenye thamani ya shilingi 1,248,100.00 kwa wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza kwa shule 5 za Msingi.
Jumla ya wanafunzi 1783 wamepatiwa maziwa hayo Ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi kupitia unywaji wa maziwa.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa zoezi na mtoaji elimu kuhusu umuhimu wa kunywa maziwa Shuleni Bwana Msafiri V. Mkunda ambaye ni Afisa Mifugo Wilaya ya Kongwa, Shule zilizonufaika na mgao huo ni Mlimagata, Manungu, Chimlata, Mnyakongo na Kongwa.
Maziwa hayo yamesindikwa katika Kiwanda cha Maziwa cha Halmashauri kilichopo katika Kijiji cha Mbande, ambapo bidhaa hiyo inatambulika kwa jina la Kongwa Maziwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.