Baada ya kukamilika kwa ufungaji wa miundombinu ya mtandao kiambo (LAN) na kusimikwa kwa mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Hospitali wa Serikali ya Tanzania (GoT-HoMIS), Hospitali ya Wilaya ya Kongwa imeanza kutumia mfumo huo rasmi tarehe 17 Mei, 2018.
Mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huu wa kielektroniki yametolewa kwa baadhi ya watoa huduma waliokuwapo wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na Kitengo cha TEHAMA cha Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI kwa siku saba - Mei 11 hadi 17, 2018.
Matumizi ya mfumo huu yanatarajia kuleta tija na kuongeza ufanisi katika masuala ya usimamizi wa dawa na vifaa tiba, pamoja na kutunza kumbukumbu nzuri ya taarifa za wagonjwa watakaofika kjupata huduma katika Hospitali ya Wilaya.
Pia, Mfumo utasaidia sana katika kuboresha usimamizi wa mapato ya Hospitali kwani unataunza taarifa za kifedha zinazokusanywa kupitia wagonjwa wasio kuwa na bima za afya na kuarahisisha upatikanaji wa takwimu mbalimbali kuhusu wagonjwa waliopata huduma katika Hospitali kwa makundi yao - wazee, watoto, bima za afya za NHIF na CHF-Iliyoboreshwa, na wasio nabima.
Pamoja na kufungwa kwa mfumo huu, kumekuwa nachangamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalam wa huduma za afya, na vifaa vya kompyuta.
Uongozi wa Hospitali unafanya jitihada za kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Hospitali hii kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wateja wake wote.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.