JUKWAA LA KUTETEA USTAWI WA MNYAMAKAZI PUNDA KUANZISHWA KONGWA
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari - Kongwa DC
Kikao cha kwanza cha kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa Jukwaa la kutetea ustawi wa mnyama kazi Punda unaotekelezwa na Shirika la INADES- Formation Tanzania na kufadhiliwa na Broke East Afrika kupitia mradi wa kuboresha Maisha ya Jamii kupitia kuboresha ustawi wa mnyama kazi Punda.
Baadhi ya wataalam walioshiriki katika kuanzishwa kwa jukwaa hilo.
Bwana George Pharles, Afisa Mradi amesema kuwa mradi huo utatekelezwa katika Vijiji vitatu vya Wilaya ya Kongwa ambavyo ni Mautya A, Nguji na Makole kwa lengo la kuongeza thamani kwa mnyama kazi punda, kuanzisha biashara ili kuinua uchumi, Kuanzisha mashamba ya malisho, kuanzisha mfuko maalumu wa kusaidia matibabu na kuanzisha Klabu mashuleni ili watoto waelewe thamani ya punda na kutoa elimu kwa wengine.
Bw Geoege Pharles Afisa mradi akitoa ufafanuzi wa mradi huo mbele ya wadau.
Pia Bw. Pharles amefafanua kuwa licha ya kuanzishwa kwa Jukwaa hilo, pia mradi utakuwa na kazi ya kusimamia uanzishwaji wa sheria ndogo ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji kwaajili ya kutetea mnyamakazi Punda.
Bi. Jacqueline Nicodemus, meneja wa mradi amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwenye biashara ya punda hivyo mradi unafanya kazi kuhakikisha haki za wanyama zinatekelezwa hususani utekelezaji wa zuio la uchinjaji wa Punda.
Bi Jacqueline Nicodemus Meneja mradi akiongea katika kikao hicho.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.