"Jumla ya ng'ombe wa asili 121,907 wa wananchi wamepigwa chapa ambayo ni sawa na asilimia 105.2% ya lengo". Haya ameeleza Dkt Omary Nkullo (Afisa Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Kongwa) wakati akiwasilisha taarifa ya Zoezi la Upigaji Chapa Kiwilaya.
Afisa Mifugo na Uvuvi (W) ameeleza kwamba; Wilaya ya Kongwa ilianza kutekeleza sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa mifugo namba 12 ya mwaka 2010 na agizo la Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kupiga chapa ng’ombe wote kuanzia tarehe 10/08/2017. Kutokana na takwimu za mifugo tulizonazo tulitegemea kupiga chapa ng’ombe 115,870 (Wa asili) wa wananchi na ng’ombe 8,927 wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na TALIRI.
Zoezi la kupiga chapa Kongwa lilihitimishwa tarehe 24/11/2017 ambapo jumla ya ng’ombe 121,907 (Wa asili) wa wananchi wamepigwa chapa ambayo ni sawa na asilimia 105.2% ya lengo. Aidha, ng’ombe wa taasisi za Serikali za NARCO na TALIRI; wizara ilitoa maelekezo kwa njia ya simu kuwa wasipigwe chapa ya vijiji na badala yake watabandikwa hereni (Ear tags).
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.