Kamati ya fedha uongozi na mipango imefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Kata mbalimbali za wilaya ya Kongwa.Baadhi ya miradi ambayo imekaguliwa ni Pamoja na ujenzi wa bweni la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kongwa ambayo ilipokea shilingi milioni Hamsini laki tatu na ishirini mwezi wa sita mwaka 2024 kwa ajili ya kumaliiza ujenzi wa bweni hilo kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita.
ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Kongwa
Akizungumza kwa niaba ya jumuiya ya shule ya sekondari Kongwa, Mkuu wa shule ameeleza kuwa baada ya kupokea fedha hizo mchakato wa awali wa kukamilisha ujenzi ulianza.
Aidha Mkuu wa shule ameeleza changamoto za kuchelewa kwa ujenzi huo ni kutokana na changamoto za mfumo wa NEST akiainisha kuwa changamoto nyingine ni upatikanaji wa maji kuwa wa kusuasua hivyo kuchelewesha zoezi la ujenzi huo.
Akiongea baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa Pamoja na matundu sita ya vyoo katika shule ya Msingi Matuli, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. Richard Mwite ameeleza kuwa Pamoja na changamoto zilizopo kwenye mfumo wa NEST ikiwemo mfumo huo kuwa bado haujazoeleka na watumiaji watendaji kazi wavumilie na wafuate masharti na michoro Pamoja na maelekezo ya ujenzi husika kwani majengo ya serikali yana wakaguzi wengi na pia ameshauri mawasiliano kati ya mafundi na wahandisi ili kuepusha kufanya ujenzi wenye dosari utakaosababisha hasara kwa serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. Richard Mwite pamoja na Viongozi wengine wakiongea na wananchi.
Aidha Mhe. Richard Mwite amewaeleza wananchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa kuhakikisha anawaletea wananchi maendeleo kwa kuleta miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kongwa hivyo wananchi waunge mkono juhudi zake ili kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inafanyika kwa viwango vya kuridhisha na inaleta maendeleo katika Wilaya ya Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.