Na Stephen Jackson, Kongwa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Bi. Pilli Mbaga amepongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Wilayani Kongwa.
Bi Mbaga ametoa Pongezi hizo wakati wa ziara ya kamati ya siasa Mkoa wa Dodoma ya kukagua ujenzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Katika ziara hiyo kamati ya Siasa ya Mkoa imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Barabara ya kiwango Cha lami ya Mwalimu Nyerere - Majengo yenye urefu wa km. 1 Kwa thamani ya Shilingi 487,199,000.00 kutoka mfuko wa Jimbo wa Barabara, Ujenzi wa Miundombinu katika Hospitali ya Wilaya wenye thamani ya Shilingi bilioni 4.64 unaohusisha Miundombinu mbalimbali zikiwemo wodi tatu za wagonjwa na Jengo la mama na mtoto.
Miradi mingine ni mradi wa Kisima Cha Maji katika Kijiji Cha Laikala "B" wenye thamani ya Shilingi 780,566,436.64 Shule ya Msingi Moleti iliyojengwa kupitia mradi wa Boost Kwa thamani ya Shilingi 318,800,000.00 na mradi wa Kuboresha umeme Kwa ajili ya kutatua kero ya umeme hafifu Kwa Wilaya za Kongwa Mpwapwa na Gairo, unaohusisha ujenzi wa njia ya msongo wa Kilovoti 33 kutokea kituo kidogo Cha Zuzu hadi Mbande wenye thamani ya Shilingi
5,104,849,344.90.Aidha katika miradi yote hiyo Kamati imetoa Pongezi za dhati na kutoa Rai Kwa Wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani imedhamiria kutatua kero zinazowakabili Wananchi.
Aihutubia Wananchi wa Kijiji Cha Moleti waliojitokeza kumpokea, Bi. Mbaga amewataka Madaktari na Wauguzi wa Hospitali hiyo kuwa na kauli nzuri kwa Wagonjwa Ili dhamira ya Serikali iweze kutumia.
Akihutubia Wananchi wa Kijiji Cha Moleti waliojitokeza kuipokea kamati hiyo katika viwanja vya Shule ya Msingi Moleti, Bi. Mbaga, amepongeza Menejimenti nzima ya Wilaya ya Kongwa kwa ushirikiano na jitihada za pamoja katika usimamizi wa miradi ya Maendeleo. "Mimi niwapongeze sana Mbunge, Mwenyekiti wa Chama, Mkuu wa Wilaya, pamoja na Serikali mfanya kazi nzuri sana" Alisema Bi. Mbaga.
Akizungumza katika Ofisi ya Chombo Cha Watumia Maji (CBWSO) Kijiji Cha Laikala " B" amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kwa kuwaletea Maendeleo Wananchi wa Kijiji hicho huku akisisitiza kukamilika mapema kwa mradi huo Ili Wananchi waweze kuondokana na kero hiyo ya muda mrefu ambapo, pia ametoa wito kwa Serikali kuboresha taratibu zake kuhusu miradi mikubwa Ili iweze kuhudumia Wananchi wa eneo Moja kwa usawa pasipo kuzingatia mipaka ya maeneo ya Kiutawala.
Mhe. Ndugai, ametolea mfano wa Mradi wa Maji katika Kijiji Cha Laikala B" unaosimamiwa na RUWASA, kuwa bajeti hiyo imeelekezwa kwenye Kijiji hicho tu huku Wananchi wa Laikala "A" Wakiachwa bila huduma Ile hali mradi huo ungeweza kuwafikia wote, jambo ambalo Bi. Mbaga ameagiza Serikali kulifanyia kazi na kufikia Mwezi Disemba, 2023 Wananchi waanze kutumia Maji ya mradi huo.
Kuhusu Suala la Umeme, Ndugai amesikitishwa na kero ya kukatika Kwa umeme mara kwa mara Hali inayodaiwa kurudisha nyuma jitihada za Wananchi katika kujiletea Maendeleo kupitia viwanda. "Tanesco ni lazima Mwende na nia aliyonayo Rais baadhi ya desturi zenu lazima zibadllike" Alisema Mbunge Ndugai.
Akizungumza kwa Niaba ya Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. White Zuberi Mwanzalila ameihakikishia kamati hiyo kuwa Kongwa itaendelea kuwa Ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na Ushirikiano mkubwa uliojengeka kati ya Chama hicho, Halmashauri, Ofisi ya Mbunge na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.
Ziara hiyo ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Dodoma imehusisha viongozi mbalimbali wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya na Mkoa, pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo (Wataalamu) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.