Na Stephen Jackson, Kongwa
Kamati ya siasa mkoa wa Dodoma imepongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi ya maendeleo wilayani Kongwa.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ndugu Godwin Azaria Mkanwa wakati wa ziara ya kutathmini utekezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020-2025.
Akisoma Taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Msingi Jobu Ndugai inayojengwa katika Kijiji Cha Chimotolo, Afisa Mtendaji kata ya Ugogoni ndugu Lister Mhagama, alisema Ujenzi huo upo katika hatua nzuri na ikiwezekana ifikapo Mwezi January 2022, shule itaanza kuupokea wanafunzi.
Kwa upande mwingine Kamati imetembelea Miradi ya vijana wajasiriamali katika Kijiji cha Hogoro Kata ya Hogoro wanaojishughulisha na miradi mbalimbali ikiwemo Ufundi chuma na uoshaji wa Magari kupitia mikopo isiyo na riba inayotolewa na Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Wakiwasilisha taarifa yao vijana hao wametaja changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kukosekanakwa umeme wa uhakika.
Kamati imepongeza jitihada za vijana hao na kuwasisitiza kutumia fedha vizuri ili waweze kujikwamua na umaskini kupitia shughuli zao.
Aidha kamati imewataka viongozi kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi na kusimamia matumizi sahihi ya mikopo hiyo.
Ziara hiyo ilitangiliwa na mkutano wa Wakuu wa Idara na taasisi za serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri, ili kujadili taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya TZS Bilioni 1.5.
Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki ni TANESCO, RUWASA, DUWASA,TARURA na TFS.
Baada ya kupitia kurasa za Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilayani Kongwa lilionesha ufanisi kwa kuunganisha umeme katika vijiji 83 kati ya 87 vya wilaya ya Kongwa.
Kufuatia ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Remidius Mwema Emmanuel ameushukuru uongozi wa kamati hiyo na kuahidi kusimamika kikamilifu Miradi yote inayotekelezwa Wilayani Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.