Na Stephen Jackson, Kongwa
Mkuu wa gereza Kongwa Sp. Tekla Erasto Ngilangwa ametoa rai kwa Maafisa na Askari wa gereza Kongwa kuzingatia weledi, bidii na uzalendo ili kujiletea mafanikio.
Rai hiyo ya Sp. Ngilangwa imetolewa Aprili 18, 2024 katika ukumbi wa gereza Kongwa, wakati akizungumza na baadhi ya Maafisa na Askari wa gereza la Kongwa na wajumbe wa kamati ya usalama wilaya ya Kiteto ikiongozwa na Mhe. Remidius Mwema Emmanuel Mkuu wa Wilaya hiyo, walipofanya ziara ya mafunzo katika gereza la Kongwa kwa lengo la kujifunza mbinu na mikakati inayotumiwa na gereza kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Kilichofanyika ni utayari wa kwetu sisi maafisa na askari, lakini utayari wa viongozi wanaotuzunguka ndani ya wilaya na kuamini kweli magereza wanaweza lakini na kikubwa zaidi uzalendo" Sp. Ngilangwa.
Aidha Sp. Ngilangwa alitoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa jeshi la Magereza Tanzania Afande Cgp Mzee Ramadhan Nyamka kwa ushirikiano mkubwa alioutoa kupitia kwa mkuu wa magereza mkoa wa Dodoma (Rpo)
Akiwasilisha taarifa maalumu ya miradi, Mkaguzi wa Magereza Ally Selestine Mugunda alisema, licha ya gereza kujihusisha na miradi mbalimbali bado linakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo ufinyu wa bajeti, ukosefu wa visima vya kuendesha miradi ya umwagiliaji n.k.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema Emmanuel licha ya kutoa pongezi nyingi kwa Viongozi wa Gereza Kongwa pia aliwataka viongozi Wilayani kiteto kutumia uzoefu walioupata kufanya mageuzi katika nyanja mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kongwa Mwl. Mussa Abdi Matari amepongeza jitihada za Mkuu wa gereza Kongwa SP. Tekla Ngilangwa kwa uhodari wake na uzalendo kwani baada ya maboresho gereza limekuwa na mvuto kiasi cha kupunguza machungu kwa wafungwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza Kiteto SP. Peter Juberk alisema, licha ya kuwepo kwa jitihada za kuboresha hali ya ustawi wa gereza katika wilaya ya Kiteto, Atatumia uzoefu alioupata Kongwa ili kufikia malengo hivyo amemuomba mkuu wa Wilaya kuunga mkono jitihada hizo.
" Nimefarijika sana kwa mambo niliyoyaona kwa macho na kwa kupitia skrini yetu pale, nakupongeza sana kwa juhudi ulizofanya kuendeleza hili gereza Kongwa, mimi naona kamati ya hapa ni ngangali hongerenj sana, siyo kuwa kule gereza kiteto hakuna kitu, no ! isipokuwa hapako kama hapa! hapa pako juu"
Tangu miundombinu ya gereza Kongwa ijengwe na wakoloni takribani mwaka 1949 yamekuwa yakitumika majengo na miundombinu chakavu, hali iliyopelekea Sp. Tekla Ngilangwa kuanzisha mchakato wa ukarabati ambao umefanya upya mwonekano wa madhali ya ndani na nje ya gereza.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.