Katika kuendelea kuhamasisha jamii kujenga na kutumia vyoo bora kupitia kampeni ya Taifa ya Usafi inayoratibiwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee, na Watoto, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa itaendesha kampeni hii siku za tarehe 6 na 7 Desemba, 2018 katika kata za Kibaigwa, Kongwa, Mkoka na Sejeli eneo la Mbande.
Kupitia kampeni hii, kaya mbalimbali zisizokuwa na vyoo zitapungua kwa asilimia kubwa.
Kauli mbiu ya Kampeni hii ni “Usichukulie poa nyumba ni choo”
Aidha, Mratibu wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya Bw. Anyitike Mwakitalima, amesema “choo bora ni choo kinachozuia kuenea kwa kinyesi katika mazingira ya binadamu, kuwa na sakafu inayosafishika kwa maji, kiwe na usiri, mlango pamoja na paa”.
Kampeni hii kwa Wilaya ya Kongwa itahusisha viongozi mbalimbali pamoja Mjomba Mrisho Mpoto kusherehesha.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.