Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel ameitaka Kampuni ya "Agricom Africa Ltd" Tawi la kibaigwa kuwakabidhi wateja wake Matrekta waliyoagiza kwaajili ya Shughuli za kilimo ifikapo Januari 5, 2022.
Mkuu huyo wa Wilaya alifika katika ofisi za kampuni hiyo Tarehe 31Disemba 2021, wakati akitokea kwenye ziara ya ukaguzi wa Madarasa 130 aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji (W) Kongwa Dr. Omary Nkullo.
Naye Meneja wa Kampuni hiyo Ndugu Peter Temu alitoa ufafanuzi kuhusu changamoto zilizopelekea malalamiko ya wateja wake, na kueleza kuwa mchakato wa kuingiza Matrekta hayo unaendelea na ifikapo Jumanne ya tarehe 4 Januari Matrekta mengine yatakuwa yamewasili.
Ndugu Temu ameongeza kuwa Katika Matawi yote Nchini Tawi la Kibaigwa ndilo pekee linaloongoza kwa mauzo na hivyo kwa niaba ya kampuni ameahidi kusaidia kuchangia Madawati kwa baadhi ya shule zilizo jirani na kampuni hiyo kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii. (Social responsibility).
Aidha Mhe. Remidius Mwema ameuasa Uongozi wa Kampuni hiyo kuongeza wigo wa kupata taarifa zinazoihusu kampuni yao ili kubaini wadau wenye nia ya ovu ya kuharibu ufanisi wa kampuni kwa udanganyifu.
Ziara ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kongwa katika ofisi hiyo, iliambatana na Kamati Kuu ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.