Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani tarehe 24 Mei, 2018, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. White Zuberi amemuomba Katibu Mkuu Utumishi kurejea kauli ya kwamba, "Mkurugenzi hana ruhusa ya kumzuia uhamisho wa mtumishi pindi anapotaka kuhama".
Katibu Mkuu Utumishi ameombwa kufuta kauli hiyo kufuatia changamoto kubwa ya kuhama kwa idadi kubwa ya watumishi kwa kipindi ambacho Halmashauri ya Kongwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa Idara mbalimbali hususani Idara za Elimu na Afya.
Mhe. White amesema Katibu Mkuu Utumishi alitoa kauli hiyo Katika Mkutano Rasmi uliyojumuisha Wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Utumishi, Wakurugezi, Maafisa Mipango, na Mameya wote.
Mhe. White anaeleza kwamba licha ya aadhi ya watumishi kupungua kwa kutolewa kutokana na kukutwa na vyeti vya kugushi (fake) wakati wa Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Hewa, kwa Kipindi cha miezi mitatu Watumishi 73 wamehama, baada ya kauli ya Katibu Mkuu Utumishi.
Alisisitiza kwamba Kauli hiyo ya Katibu Mkuu Haitendi haki kwa Halmashauri ya Kongwa na zingine Nchini kote hasa zilizopo pembezoni na hali inayoleta hofu ya maeneo yaliyopo pembezoni Kukosa wafanyakazi kwani watakuwa wakihama kuhamia mjini na kukwepa maeneo ya vijiji vya Pembezoni.
Kadhalika ameeleza kuna baadhi ya maeneo watumishi walikuwa wakigoma kwenda, lakini Halmashauri ilikuwa ikiwapa motisha ili waweze kuvumilia kuishi, hivyo, tafsiri ya kauli hiyo ya Katibu Mkuu inasababisha watumishi wengi waliopo maeneo yenye Changamoto kuhamia mjini na kuendelea kuongeza Tatizo la upungufu wa watumishi.
Hivyo, Katibu Mkuu anapaswa Kutengua Kauli hiyo, na suala la uhamisho aliomba aachiwe Mkurugenzi kuhamisha watumishi wenye sababu ya msingi tu, kwani haitakuwa busara kuomba watumishi kupitia Bajeti, Halafu wahame kiholela, pia utendaji wa huduma kwa wananchi utapungua Sana na Kusabisha lawama kwa Serikali.
Aidha, alisema Tayari Serikali imeshaleta idadi ya watumishi watakaoajiriwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambapo Halmashauri ya Kongwa imepitisha nafasi 600 za ajira, lakini Kauli hiyo Kama itaendelea kutumika basi hata wakiajiriwa watumishi wengi bado wataendelea kuhama na ukubwa wa Tatizo kubaki pale pale.
Madiwani kutoka Kata Mbalimbali za Halmashauri ya Kongwa kwa pamoja wameunga mkono Hoja hii na baadhi yao wanasema wana matumaini Katibu Mkuu ataridhia na hatimaye Kufuta kauli hiyo.
Diwani wa Kata ya Mlali, Mhe Richard Mngurumi ameeleza kwamba Zahanati ya Ihanda katika Kata yake imefungwa baada ya mtumishi aliyekuwapo kuhama, licha ya mtumishi mmoja kuondolewa kutokana na sakata la vyeti vya kugushi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.