KATIBU TAWALA MKOA DODOMA AMEFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI KONGWA
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari - Kongwa DC
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Khatibu Kazungu amefanya ziara ya kikazi Wilayani Kongwa leo Septemba 15, 2025 akiwa na lengo la kujitambulisha na kuongea na watumishi.
Akiongea na watumishi wa Wilaya ya Kongwa katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Veta Kongwa Bw. Kazungu amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa kuheshimiana, kuzingatia sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma kwani hiyo ndiyo miongozo inayosimamia utendaji wa watumishi wa kazini.
Bw. Khatib Kazungu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Aidha Bw. Kazungu amesisitiza watumishi kuzingatia malengo ya dira ya taifa ya mwaka 2050 na ilani ya Chama cha Mapinduzi kinachotawala chini ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
"naomba ushirikiano ili tuweze kulisongesha gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Dodoma na niwahakikishie kila mwenye changamoto aje kuniona" amesema Kazungu.
Baadhi ya Watumishi wilaya ya kongwa wakiwa katika mkutano huo.
Akisoma taarifa ya Maendeleo ya Wilaya Katibu Tawala Wilaya ya Kongwa Bi. Sozi Ngate amesema kuwa Wilaya ya Kongwa inaendelea vizuri na mashirikiano mazuri baina ya Taasisi, Chama na Wananchi na wanaahidi kushirikiana nae katika kutimiza wajibu wao katika kazi.
Katibu Tawala Wilaya ya Kongwa Bi. Sozi Ngate akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Wilaya ya Kongwa.
Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wamesema wamempokea na kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma na wanaahidi kushirikiana nae katika safari ya kuelekea 2030.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo akiwa katika mkutano huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.