Kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) kimefanyika huku kikiwa na ajenda mbalimbali ikiwemo Kupokea na Kujadili taarifa za Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2024/25
Aidha kamati imepokea na kujadili taarifa ya vyama vya Ushirika Wilaya ya Kongwa kwa mwaka 2024/2025 pamoja na kujadili kuhusu Usajili wa Wafanya biashara Wadogo ambao umetekelezwa katika Kata Mbalimbali za Wilaya ya Kongwa.
Akizungumza kuhusiana na Lengo la usajili wa wafanyabiashara, mjumbe wa kamati ameeleza kuwa dhumuni la usajili huo ni Kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara ndogondogo ili wafanyabiashara hao waweze kunufaika na Fursa mbalimbali ambazo zinatokana na Utambuzi unaoletwa na vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo (machinga);
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.