Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF III) kwa utekelezaji wa awamu ya kwanza unaondelea kufanyika nchini kote umeonyesha mafanikio makubwa katika juhudi za kunusuru kaya masikini. Mafanikio hayo yameonekana kuleta tija kwa walengwa na yamejipapazua bayana pale timu ya wataalam wa Kitengo cha TASAF Kongwa ilipofanya ziara kupata picha halisi ya namna ambavyo walengwa wameweza kunufaika na kuinua hali zao za kimaisha kama ilivyothibitishwa na Mkazi wa kijiji cha Iduo, Kata ya Iduo, Wilaya ya Kongwa, Anderson Andrea Kusalula mlengwa mwenye umri wa miaka 56 (010301010104842).
Mlengwa huyo alipohojiwa kuhusu mafanikio aliyoyapata toka aanze kupokea ruzuku ya kunusuru kaya maskini alisema, hadi sasa amepokea awamu 22 tangu mpango wa kunusuru kaya masikini uanze kutekelezwa Wilaya ya Kongwa, Yeye hupokea ruzuku ya Tshs. 44,000 kila baada ya miezi miwili (2), ambapo Tshs. 20,000 ni ruzuku ya msingi, Tshs. 8,000 ni ruzuku ya ziada, Tshs. 8,000 ni ruzuku ya mtoto mmoja anayehudhulia kliniki na Tshs. 8,000 ni ruzuku ya watoto wanao soma shule ya msingi.
Kwa shuhuda zaidi soma makala ya "UHAKIKA WA CHAKULA HUONDOA UMASIKINI.pdf"
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.