KOFIH YAKABIDHI VIFAA NA MIUNDOMBINU YA AFYA KONGWA
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa imekabidhiwa jenereta moja pamoja na majengo mawili ikiwemo jengo la kliniki ya huduma za uzazi na mtoto pamoja na jengo la wodi ya watoto katika kituo cha Afya Kibaigwa kupitia ufadhili wa Serikali ya Korea kupitia Taasisi ya Kimataifa ya kuboresha afya “Korea Foundation International Healthcare” (KOFIH).
Katika Mkoa wa Dodoma, kiasi cha takribani Shilingi Bilioni 5.524 katika kipindi cha miaka minne kimetolewa na KOFIH ambapo fedha hizo zinatajwa kutumika kuboresha mazingira ya utoajihuduma za afya kwenye vituo vya mradi ambao unatekelezwa katika Wilaya mbili za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Kongwa na Mpwapwa.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya kongwa walioshiriki katika hafla ya makabidhiano hayo.
Akiongea mbele ya mgeni rasmi, mwakilishi mkaazi wa KOFIH Bw. Gyeongloae Seo, ameleza kuwa majengo ambayo wameyakabidhi pamoja na jenereta yana lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watafurahishwa kuona majengo hayo yanatumika ipasavyo na kuwa na athari chanya katika jamii ya wanakongwa na watanzania kwa ujumla.
Bw Gyeongloae Seo mwakilishi mkaazi wa KOFIH akiongea katika hafla ya makabidhiano.
Naye mkuu wa wilaya ya kongwa mhe. Mayeka s mayeka amewashukuru KOFIH kwa ufadhili huo wakati akikabidhiwa majengo hayo pamoja na jenereta na kuongeza kuwa ufadhili huo unakuja baada ya juhudi za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha mahusiano mazuri nan chi za nje hivyo haya ni matunda ya Nchi ya Tanzania kuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingine.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.