Na Stephen Jackson, Kongwa
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amewapongeza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Shule ya Sekondari Lenjulu kupitia mradi wa SEQUIP.
Kwa mujibu wa Mhe. Ndejembi, Halmashauri mbalimbali nchini zilipewa kiasi sawa cha fedha kujenga shule mpya za kata ambapo Kongwa ilipatiwa kiasi cha shilingi Mil. 470 na iliweza kukamilisha ujenzi wa shule hiyo na hivyo kuwa ni Halmashauri ya kwanza Nchi nzima kukamilisha ujenzi kwa bajeti tengwa.
Ndejembiaameeleza kuwa Maeneo mengine hadi Sasa hayajakamilisha ujenzi huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutotosheleza kwa bajeti ya fedha zilizotolewa.
Awali Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Omary Nkullo aliwasilisha taarifa ya mradi huo ambayo inaeleza mbinu zilizotumika kukamilisha mradi huo Kwa fedha sh. mil. 470 ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Kamati tatu za usimamizi.
Diwani wa Kata ya Lenjulu Mhe. Briton Chisongela alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuongeza Idadi ya Walimu ili kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi wa kata hiyo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Ndejembi amezungumza na Wanafunzi wa shule hiyo na kuwataka kuongeza bidii katika maomo yao ili waweze kufaulu mitihani yao.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.