Na Mwandishi Wetu, Kongwa.
Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utanaduni wa Afrika ya kusini Mhe. Nocawe Mafu amesema Nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala yote yanayohusu historia ikiwa ni pamoja na kushiriki matamasha ya utamaduni kuhusu Ukombozi wa bara la Afrika.
Mhe. Mafu amebainisha hayo wakati alipotembelea Masalia ya Kambi ya wapigania Uhuru Wilayani Kongwa kwa lengo la kuyatambua Maeneo ya kihistoria ya ukombozi wa Afrika ya kusini.
Katika Hotuba yake alitoa shukrani za dhatu kwa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa uamuzi wake wa kutoa eneo la Kongwa kama sadaka kwa nchi za Afrika litumike kwenye harakati za Ukombozi.
" No Mazimbu, no Dakawa without Kongwa" Alinukuliwa Mafu.
Aliongeza kuwa ni vema vizazi vikatambua umuhimu wa Tanzania kupitia Jitihada za Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere za kuitambua thamani ya Watu wa Nchi za Afrika Kusini, Angola, Zimbabwe, Namibia na Msumbiji.
Naye Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Ms Noluthando Mayende Malepe alisema Kongwa ni eneo la muhimu ambalo haliwezi kufutika katika historia ya ukombozi wa nchi za Afrika hivyo watalienzi kwa hali na mali ili historia yake idumu vizazi na vizazi.
Ziara ya Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utanaduni wa Afrika ya kusini Mhe. Nocawe Mafu Wilayani Kongwa ilipokelewa na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, na itahitimishwa na kongamano la msimu wa tamasha la utamaduni wa watu wa Afrika Kusini ambalo linatarajiwa kufanyika Zanzibar.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.