Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Kununuliwa kwa vifaa vya kisasa vya Upimaji wa Ardhi Wilayani Kongwa kutapelekea mapinduzi makubwa ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wananchi ikiwemo ujenzi holela.
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya makazi, imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kutatua migogoro ya Ardhi kote Nchini na kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa za kumilikishwa Ardhi na kuiendeleza sanjali na kujipuesha na ujenzi holela.
Makampuni kadhaa yamekuwa yakishirikiana na Serikali kurasmisha maeneo ya makazi na kupima Ardhi kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za jamii. Hata hivyo changamoto kubwa imekuwa ni uwezo hafifu wa baadhi ya Halmashauri wa kutokuwa na vifaa vya Uhakika vya Upimaji Ardhi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imejizatiti kuhakikisha tatizo la ujenzi holela linakuwa Historia, na ndiyo sababu ilifanya maamuzi magumu ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kupima Ardhi ambavyo tayari vimewasili na kufanyiwa majaribio ambayo yalitoa matokeo chanya.
Katika baraza la Madiwani la tarehe 10 Februari 2023, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary A. Nkullo aliwaeleza wajumbe kuwa Divisheni ya Ardhi imefanikiwa kununua vifaa vya kisasa vya kupima Ardhi ambavyo vina uwezo mkubwa kuliko makadirio ya awali.
Alisema Kifaa hicho kinachoitwa RTK kilichonunuliwa ni cha kisasa Sana chenye uwezo wa kupima umbali wa km 20 na Hivyo baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa linaandika rekodi ya kuwa miongoni mwa Halmashauri chache zenye vifaa vya kisasa vya Upimaji Ardhi.
"Wakati tunapata specifications, tuliandika km. 8 kwenye specifications lakini yule bwana ametuletea yenye km. 20" - Dkt. Nkullo.
Ameongeza kuwa awali Halmashauri ilikuwa ikikodishwa kifaa Cha Upimaji kwa thamani ya shilingi 300,000.00 kwa Siku, Sasa endapo baraza litaridhia kifaa hicho pamoja na kutumiwa na Divisheni ya Ardhi pia kinaweza kukodishwa maeneo mengine na kuwa sehemu ya vyanzo vya mapato ya ndani.
Kwa hali hii kuna Kila sababu ya kuupongeza uongozi mzima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuanzia mwenyekiti wake Mhe. White Zuberi Mwanzalila, Makamu wake Mhe. Richard Mwite, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Wilaya ya Kongwa Dkt.Omary A. Nkullo, waheshimiwa Madiwani wa Kata zote 22 za Wilaya ya Kongwa na Kamati zote za Madiwani pamoja na wakuu wa Divisheni, vitengo na Seksheni.
Kila jambo hutegemea zaidi uthubutu ndipo liweze kufanikiwa. Ni lazima jitihada hizi za kubuni namna ya kutatua changamoto kwa kubaini vipaumbele zitiliwe mkazo Kwa kila changamoto ndipo mafanikio yatakapofikiwa.
Dkt. Nkullo alisisitiza kwamba seti ya vifaa hivyo vya kisasa (RTK) ni yenye thamani kubwa ingawa hakuitaja amesema ni lazima vitunzwe kwa umakini na uangalizi mkubwa Ili viweze kudumu na Hivyo kuleta tija kwa manufaa ya umma.
Wajumbe wa baraza la Madiwani, walipiga makofi ishara ya kushangilia mafanikio ya Halmashauri, kinachosuburiwa Sasa ni matokeo ya utatuzi wa changamoto za ardhi. Kufikia azma hiyo itawalazimu watumishi wa Divisheni hiyo kujituma kwa kila hali Ili kuleta tija iliyokusudiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.