Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mji Mdogo wa Kongwa inatekeleza mradi mkubwa wa maji ambao utanufaisha wakazi waapatao 29,039 ambayo ni sawa 90% ya wakazi waliopo Kata za Kongwa, Ugogoni, na sehemu ya Kata ya Sejeli.
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kongwa, Eng. Kaitaba Lugakingira akizungumza na Afisa TEHAMA (W), ameeleza kwamba hali halisi ya utoaji wa huduma ya maji kwa sasa ni asilimia 47.4 (47.4%) katka mji wa Kongwa, hivyo mradi huu utakuwa mwarobaini kwa changamoto za maji zilizokuwa zikiusumbua mji wa Kongwa.
Aidha, ameeleza kwamaba mradi huu unagharimu TSh. 1,549,168,228.17 (Shilingi bilioni moja milioni mia tano arobani na tisa mia moja sitini na nane elfu mia mbili ishirini na nane na senti kumi na saba) ikijumuisha 18% ya Kodi ya Ongezeko la thamani (18%VAT).
Mradi unatekelezwa na Mkandarasi HEMATEC INVESTMENT LIMITED wa S.L.P 34078, DSM, ambaye ameshaanza kazi baada ya kusaini mkataba tarehe 25/01/2018 na anatarajia kukamilisha mradi tarehe 08/09/2018.
Mradi unasimamiwa na Mhandisi wa Maji wa Wilaya Kongwa na Mkandarasi amepangiwa kufanya kazi zifuatazo;
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.