Sekta ya Elimu katika Wilaya ya Kongwa ni sekta ambayo inahudumu kundi kubwa la wananchi wote Wilayani na inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya madarasa, maabara, nyumba za walimu na samani.
Hivyo, Baraza la Madiwani lemefanya Mkutano maalum kujadili changamoto hizo na kuweka mikakati ya kuinua kiwango cha elimu katika Wilaya ya Kongwa ili kuifanya Kongwa kuwa Wilaya ya kwanza katika Jiji la Dodoma.
Katika majadiliano, Baraza limeona kwamba michango kutunisha mfuko wa Elimu ndiyo itasaidia kukabilana na changamoto zilizotajwa hapo juu kupelekea kuboresha utoaji wa taaluma shuleni na kuinua ufaulu kwa ujumla.
Baraza limetoa utaratibu wa uchangiaji ambapo kila mkazi mwenye uwezo wa kfanya kazi katika Kata atachangia Tsh. 10,000/= kwa mwaka ambazo zitaingizwa kwenye akaunti ya Kata kwa ajili ya maendeleo ya elimu.
Kamati za maendeleo za Kata zitapokea mahitaji ya matumizi kutoka katika vijiji kulingana na michango yao kutokana na mahitajiya kielimu katika shule za Msingi na Sekondari
za Kata hiyo; matumizi yataidhinishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Aidha, imeelezwa kwamba hatua hizi ni taratibu za awali katika kufikia kuwepo kwa mfuko wa elimu wa Wilaya ambao unasubiri sheria ikamilike.
Pia, katika Baraza hili limehusisha Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ambapo Mkuu wa Wilaya Mhe. Deogratius Ndejembi ameeleza kwamba pamojana kufanya vizuri kwa Wilaya kimkoa katika mitihani iliyopita, Wilay haipo katika nafasi nzuri kitaifa, hivyo, jitihada zifanyike katika kuifanya Wilaya ya inakuwa katika nafansi nzuri zaidi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.