Wilaya ya Kongwa yafanya Mkutano wa Pamoja wa Baraza la Biashara la Wilaya na Baraza la Madiwani Wilayani Kongwa. Katika Mkutano huu Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi (Mwenyekiti wa Baraza la Biashara) amewahasa wajumbe wa mabaraza yote mawili -sekta ya umma na sekta binafsi kujikita kwenye mradi wa ufugaji kuku.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ameeleza elimu ambayo wataalam wanayo na wadau mbalimbali wa biashara waliyopewa kuhusu ufugaji kuku washirikiane katika kuisambaza kwa wananchi katika kata zote zilizopo Wialayani kongwa. Hayo ameeleza wakati wa kufunga Mkutano huo ambaomumefanyika tarehe 20 Desemaba, 2017.
Katika Mkutano huo mada mbalimbali zimewasilishwa na kujadiliwa ikiwemo; Mafanikio ya na Changamoto za Baraza la Biashara la Wilaya kwa mwaka 2017; Uanzishaji wa Dira ya uwekezaji kwa Wilaya ya Kongwa' na Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuku Mbande.
Katika taarifa ya mafanikio na changamoto imeelezwa kwamba Baraza la Biashara kwa mwaka 2017 limepata mafanikio yafuatayo;
Kuhusu Uanzishaji wa Dira ya uwekezaji kwa Wilaya ya Kongwa, imeelezwa kwamba Dira hiyo itatumika kama chanzo cha habari za uwekezaji katika Wilaya ya Kongwa, ikionesha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo, mahitaji ya uwekezaji katika fursa hizo, hatua kadhaa za kufuata, matarajio mbalimbali, kiwango cha nguvu kazi inayopatikana, miundombinu, taratibu za umiliki ardhi, masoko, huduma mbalimbali zilizopo katika maeneo ya uwekezaji n.k.
Kuhusu Mradi wa Ufugaji kuku Mbande, imeelezwa kwamba ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na LIC katika Wilaya ya Kongwa; Wazo la mradi lilitokea katika Idara ya Mifugo na Uvuvi. Mradi huu upo katika mfumo wa kongano (Cluster) ambapo wadau mbalimbali wanahusika katika utekelezaji wa mradi huu. Wadau wanaohusika katika kutekeleza mradi huu ni pamoja na wafugaji wa kuku, wauzaji wa pembejeo zinazotumika katika ufugaji wa kuku kama vile vyakula, vyombo vya chakula na maji, wauza madawa na wauza vifaranga. Mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kwa awamu kuanzia Julai 2017.
Aidha, Kikao hicho cha pamoja kimetoka na maazimio mbalimbali katika kufanya Baraza la Biashara la Wilaya kuwa endelevu pamoja na uboreshaji wa mazingira ya kiuwekezaji wilayani Kongwa; Makubaliano haya ni:-
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.