Na Stephen Jackson, Kongwa.
Mwenge wa Uhuru wilayani Kongwa umeweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya Maendeleo, kuzindua mradi mmoja na kutembelea miradi miwili kwa malengo Maalum.
Miradi iliyowekwa mawe ya Msingi ni ule wa jengo la huduma za dharula la Hospitali ya Wilaya ambao hadi sasa umetekelezwa kwa thamani ya Tsh. 292,346,696.00 kati ya 300,000,000.00 zilizotolewa na Serikali kupitia mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 na mradi wa kisima Cha Maji katika Kijiji cha Ijaka Kata ya Sagara wenye thamani ya Tshs. 104,591,646.00.
Wakati wa ziara, Mwenge wa uhuru 2022, umetembelea mradi wa vijana Twende pamoja wasakatonge unaojihusisha na uoshaji wa magari na vyombo vingine vya usafiri kupitia mkopo wa Tsh. 7,000,000.00 kutoka Halmashauri, huku shule shikizi ya Msingi katika Kijiji cha Ibwaga ikikabidhiwa mabati na kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa ndugu Sahili Nyanzabara Ghararuma.
Katika hatua nyingine Mwenge wa uhuru umezindua kituo cha kurusha Matangazo ya Redio cha Zabibu FM wenye thamani ya Tshs.117,000,000.00 ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma amefikisha ujumbe wa Sensa kupitia matangazo ya Moja kwa Moja kituoni hapo kuashiria kituo hicho kutambulika rasmi.
Aidha katika ujumbe wa Mwenge uliotolewa katika Kijiji Cha Mlali na Kibaigwa, wananchi wamehamasishwa kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa kwa kuhesabiwa mara Moja, kupinga vitendo vya rushwa wakati huo huo wakichukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)
Mkesha wa Mwenge wa uhuru umepangwa kufanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Kibaigwa.
Ziara ya Mwenge wa uhuru itaendelea tarehe 24 Agosti, 2022 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel ataukabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule mapema asubuhi katika eneo la mkesha, ambaye naye atamkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa katika eneo la makabidhiano Wilayani Gairo. .
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.