Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC Project) umeendesha mkutano wa kuwasilishaji wa mada ya Mfumo wa Kurasimisha Biashara Ndogo Katika Ngazi ya Halmashuri wilayani Kongwa. Uwasilishaji huu umefanyika kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza la Madiwani na wajumbe wa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) katika Ukumbi wa MIkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Mwakilishi wa wa LIC Ndugu Goodluck Mghonu ameeleza kwamba lengo la uwasilishaji huu ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika Wilaya ya Kongwa kwan kuna changamoto nyingi ambazo wameziona wakati wa utafiti wao. Aidha, alieleza kuwa asilimia themanini (80%) ya biashara zilizopo Kongwa si rasmi na zinapelekea ukosefu wa fursa nyingi kwa Halmashauri na wafanyabiashara wenyewe.
Mada ya mkutano amewasilisha Dr. Goodluck C. Urassa Mkurugenzi wa Chuo cha Usimamizi na Uendelezaji wa Ujasiriamali kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Aidha, mjadala kuhusu changamoto mbalimbali na ubainishaji wa makundi na biashara ndogo uliefanyika na hatimaye washiriki kuazimia masuali ya kimkakati katika kutekeleza mfumo baada ya Menejimenti kuridhia mfumo wasilishwa. Utekelezaji wa Mfumo wa Kurasimisha Biashara Ndogo kwa ngazi ya Halmashauri utaanza mara tu baada ya Baraza la Madiwani kuridhia Mfumo huu, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. White Zuberi Mwanzalila ameiagiza Menejimenti kuaharakisha utaratibu kwa kuwasilisha mada katika vikao vyote vya kamati husika na hatimaye kwenye Baraza la mwezi huu na siyo kusubiri Baraza la mwezi wa kumi.
Pia, washiriki walipendekeza kuundwa kwa kikosi kazi kitakachoshughulikia masuala yote yaliyokubaliwa ambapo ilikubaliwa kwamba Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuregenzi Mtendaji na Afsa Biashara wa Wilaya ndiyo watahusika kupatikana kwa wajumbe wa kikosi kazi na Afisa Biashara ndiye aatkuwa Mratibu kuunganisha mawasiliano na LIC, na LIC wamesema kwamab wako tayari kusaidia katika kutekeleza shughuli zote za kurasimisha biashara ndogo na Halmashauri ichangamkie fursa hii.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.