Wilaya ya Kongwa imepokea mwenge wa Uhuru, mapokezi yaliyofanyika katika viwanja vya Amani Kibaigwa. Akizungumz wakati akikabidhi mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima ametoa shukrani zake za dhati kwa viongozi na wananchi wa Morogoro ambao wameonyesha ushirikiano mzuri toka siku walipopokea mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Pwani. Pia Mhe. Malima amewashukuru wakimbiza mwenge kitaifa wakiongozwa na ndg. Ismail Ussi na kuongeza kuwa wamekimbiza mwenge katika Mkoa wa Morogoro kwa ufanisi na umahiri mkubwa kabisa.
Akiongea wakati akipokea mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameeleza kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoa wa Dodoma utakimbizwa kwatika Wilaya Saba na Halmashauri zote nane umbali wa kilomita 1333 ambapo utakagua, kutembelea, kuweka mawe ya msingi, na kuzindua miradi 56 yenye thamani ya shilingi billioni sitini na moja na milioni mia moja na kumi.
Baada ya kupokea mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amemkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka ambaye ameeleza kuwa mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Wilaya ya Kongwa na kukagua, kutembelea na kuzindua miradi yenye thamani ya shilingi billioni thelathini na tisa na milioni mia tatu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.