Na Bernadetha Mwakilabi,
Kongwa mmefanya vizuri sana katika miradi yote iliyoahidiwa kwa wananchi imetekelezwa na hii inatokana na kuwa na mashirikiano mazuri kati ya serikali na chama cha mapinduzi CCM" Amesema Mejiti.Mwenyekiti wa kamati ya siasa mkoa wa Dodoma ndugu Donald Mejiti akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati hiyo ametoa pongezi hizo katika ziara yake wilayani Kongwa ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopangwa kufanywa katika kipindi cha mwezi Januari hadi June mwaka huu kwa fedha za mapato ya ndani zaidi ya milioni 800,Ndg Mejiti amesema kuwa miundombinu hiyo iliyojengwa na vifaa bora vilivyonunuliwa vitumike ipasavyo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi kuboresha utoaji wa huduma kwa kuwa na kauli nzuri ili kuleta tija kwa wananchi.Licha ya kuagiza mwenyekiti wa halmashauri ya Kongwa na diwani wa kata ya Ugogoni kukutana na wazazi kuwahimiza juu ya umuhimu wa elimu lakini pia amesisitiza wazazi kupeleka watoto wao shule kuacha dhana potofu na badala yake wapende elimu ili vifaa na majengo mazuri ya shule yanayojengwa yawe na thamani kwao.Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa Dr Omary Nkullo amesema kuwa fedha zilizotekeleza miradi hiyo ni sehemu ya agizo la Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kuwa halmashauri zote nchini kutenga fedha za mapato ya ndani ambazo ni fedha za wananchi 40% kwaajili ya matumizi ya miradi ya maendeleo.Nae mganga mkuu wa hospital ya wilaya Kongwa Dr Thomas ameeleza kuwa fedha hizo zimefanikisha kununua vifaa tiba katika hospital ya wilaya vituo vya afya 4 na zahanati 2 ambapo upatikanaji wa vifaa hivyo umesaidia kupunguza rufaa kutoka 150 Januari - septemba 2023 hadi kufikia rufaa 90 oktoba 2023 - mei 2024.Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Kongwa wametoa shukrani zao kw Mh Rais Dr Samia Kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu afya kununua vifaa tiba na kuajiri watumishi kutoa mikopo Kwa vijana wanawake na wenye ulemavu na kuahidi kuwa watashiriki vema uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kuanza hivi karibuni.Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa chumba 1 cha maabara katika shule ya sekondari Laikala ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 8 katika shule ya sekondari Ibwaga ujenzi wa barabara ya lami nyepesi ya kilomita 0.4 ununuzi wa vifaa tiba katika hospital ya wilaya Kongwa na kikundi cha vijana wa bodaboda waliokopeshwa fedha na halmashauri ya Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.