KONGWA YAPUNGUZA IDADI YA WASIOJUA KUSOMA KUANDIKA NA KUHESABU
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari -Kongwa DC
Idara ya Elimu Msingi Kitengo cha Elimu Watu Wazima Wilaya ya Kongwa imepongezwa kwa kupunguza idadi ya watu wazima wasiojua kusoma kuhesabu na kuandika kwa 30% ikiwa imepungua kwa 8.3% kwa takwimu ya sensa ya mwaka 2012 ambapo ilikuwa na 38.3%.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kongwa Bw Sudi Abdul alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi yaliyokuwa na kaulimbiu “kukuza kisomo katika zama za kidigitali kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu” yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya hogoro ambapo ameeleza kuwa kwa karne hii ya sayansi na teknolojia ni aibu mtu mzima kutokujua kusoma kuandika na kuhesabu.
Mgeni Rasmi, Afisa elimu Sekondari Wilaya ya Kongwa Bw. Sudy Abdul akiongea na Wananchi wa Kata ya Hogoro
Bw Abdul amefafanua kuwa elimu ya watu wazima sio kujua kusoma kuandika na kuhesabu tu lakini ni pamoja na kupata stadi mbalimbali za Maisha ili kupata maendeleo kama vile stadi za kilimo, ushonaji, na biashara.
Aidha bw Abdul ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanawapeleka shule Watoto wote waliopo nyumbani kwani bado kuna wimbi kubwa la watoto wasiosoma ili kurahisisha utekezaji wa program ya Mpango wa Elimu kwa Watoto Waliokosa (MEMKWA).
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Hogoro walioshiriki katika maadhimisho hayo
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kongwa Afisa Elimu Sekondari Bi Magreth Temu amewataka Wananchi kukitumia kituo cha Elimu ya Watu Wazima kilichopo Kata ya Hogoro kupata elimu na ujuzi wanaouhitaji ili kuwasaidia kupata kipato cha familia zao.
Bi Margreth Temu Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Kongwa akiongea na Wananchi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji.
Pia bi Temu amehimiza jamii kutumia fursa za maendeleo ya kiteknolojia kupata mawasiliano na kukuza uchumi na sio kutuma matusi na mambo yasiyofaa.
Pamoja na hayo nae Bi Jane Lutego Afisa Elimu watu wazima Wilaya ametaja changamoto zinazokabili utekelezaji wa elimu watu wazima kuwa ni pamoja na mwitikio hafifu wajamii, kutoungana kwa wataalam wanaoshughulikia elimu hiyo na uwezeshaji hafifu wa shughuli za elimu ya watu wazima.
Afisa elimu watu wazima Wilaya akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.