Wananchin wa Wilaya ya Kongwa wanapaswa kuzingatia mambo ya msingi hususani matumizi ya vyoo bora ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza na mlipuko kwa ajili ya kujenga Tanzania ya Viwanda pasipokuwa na adui mkubwa wa maradhi.
Haya yamesemwa na Mhamasishaji wa Kitaifa wa "Usichukulie poa, Nyumba ni Choo" Mjomba Mrisho Mpoto katika kampeni ambayo imefanyika Kongwa katika maeneo ya Kata ya Sejeli na Kongwa Mjini.
Aidha, Mkataba wa makubaliano wa "Tamko la Kuhakikisha Kaya zote katika Wilaya ya Kongwa zinakuwa na vyoo bora na kuvitumia" umesainiwa. Mkataba huo umeitaka Wilaya ya Kongwa kufikia tarehe 25 Desemba, 2018 kila kaya iwe na choo bora na kukitumia na umeagiza viongozi wote wanaohusika katika kila ngazi ya wilaya, tarafa, kata, vijiji au mitaa na vitongoji kusimamia kikamilifu agizo hili.
Pia, Tamko linaitaka taarifa ziwe zinatolewa kila wiki, na hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo kwakuwa anahatarisha afya na uhai wake na wa watu wengine.
Tamko hili limesainiwa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Audiphace C. Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya na Ndugu Hamisi Y. Sombwe kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kongwa.
Wananchi wote tubadilike, " UCHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO"
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.