Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, amewataka wanafunzi wa ngazi ya Elimu msingi kujenga utaratibu wa kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi yao na watu wasio waaminifu.
Walimu wa S/M Chimlata wakimsikiliza Mhe. Mayeka S. Mayeka Mkuu wa Wilaya ya Kongwa akizungumza na wanafunzi.
Mhe. Mayeka alisema hayo Aprili 24, 2024 wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Chimlata muda mfupi kabla ya uzinduzi wa kampeni ya utoaji chanjo ya saratani mlango wa kizazi iliyofanyika kiwilaya shuleni hapo ngazi ya Wilaya.
Mhe. Mayeka, muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa S/M Chimlata.
DC Mayeka aliwahimiza wanafunzi lengwa wa chanjo ya HPV inayotolewa na Wizara ya Afya kuwa ni chanjo salama na haina madhara yoyote kwa mujibu wa wataalamu wa Afya." Kama chanjo hii ingekuwa na madhara, tusingeruhusu itolewe" DC Mayeka.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Mkuu wa Divisheni ya Afya, lishe na ustawi wa Jamii Daktari Thomas Ndalio alimwomba Mhe. Mayeka kuzubgumza na wanafunzi hao masuala mbalimbali, kubwa zaidi likiwa ni msisitizo wa chanjo ya HPV.Bwana Cosmas Mlimira - Mratibu wa Chanjo Wilaya ya Kongwa akitoa ufafanuzi wa Chanjo ya "HPV" mbele ya wanafunzi wa S/M Chimlata.
Naye mratibu wa chanjo (DIVO) Wilaya ya Kongwa bwana Cosmas Mlimira alisema chanjo ya HPV hitolewa kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka tisa ili kuwakinga na uwezekano wa kupata maambukizi ya vimelea visababishavyo saratani ya mlango wa kizazi pindi wanapofikia umri wa utu uzima.
Mhe. Mayeka akishudia zoezi la utoaji chanjo ya "HPV" kwa wanafunzi - S/M Chimlata
Katika hafla hiyo jumla ya watoto wa kike 179 wa shule hiyo walipata chanjo.
Aidha hadi kufikia tarehe 25 Aprili 2024, Wilaya imeweza kuvuka lengo kwa kuchanja watoto 44,542 ambayo ni sawa na 110.8% ya walengwa 40,195 waliokusudiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.