Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa leo imezindua Baraza lake jipya la Wafanyakazi baada ya lile la awali kuisha muda wake.
Uzinduzi huu ulifanyika baada ya uchaguzi kufanyika wa kuchagua wajumbe wapya pamoja na katibu mpya, ambapo Mwalimu Mbeyu Ramdhani alishinda kwa kura 29 dhidi ya kura 24 alizozipata Ndugu Unambwe Erasto (Mchumi). Hata hivyo, Ndugu Erasto alifanikiwa kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza hili jipya la Wafanyakazi. Aidha, kwa mujibu wa sheria za Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji (W) ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, hivyo kwa sasa ni Mhandisi Ngusa Izengo.
Aidha, kabla ya uzinduzi wa baraza wajumbe waliopata wasaa wa kupewa semina fupi ya majukumu mabalimbali ya baraza.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa baraza hili, alikuwa Ndugu Audifasi Mushi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa (DAS). Aidha, mgeni rasmi wakati akizindua baraza alieleza kuwa kila mjumbe katika baraza la wafanyakazi ana nafasi sawa bila kujali cheo cha mwenzake, hivyo, wajumbe watumie nafasi hii katika mvikao vya baraza ili kuweza kuishauri vema Menejimenti ya Halmashauri katika kutatua changamoto mbalimbali za wafanyakazi.
Pia, aliwakumbusha wajumbe kuwa suala la kufuatilia michango katika mifuko ya hifadhi za jamii ni suala la mtumishi binafsi, hivyo wasisubiri muda wa kustaafu ukaribie ndiyo wafuatilie michango hiyo. Kila mtumishi anapopata fursa ya kufika katika mfuko aliojiunga basi ni vema kuangalia taarifa zake za uchangiaji na endapo atagundua tatizo basi atoe taarifa mapema sehemu husika ili liweze kutatuliwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.