Wilaya ya Kongwa imeweka historia baada ya kuzindua upya Baraza la Biashara la Wilaya (Kongwa – DBC) ambapo kikao cha uzinduzi kimefanyika tarehe 25 Mei, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.
Uzinduzi huu umefanyika kutokana na baraza la awali kuvunjwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius John Ndejembi (tarehe 2 Februari, 2017). Ilielezwa kuwa sababu za kuvunjwa kwa Baraza la awali ni kutokuwa na uwakilishi mpana wa wajumbe kutoka sekta binafsi na baraza kuundwa na wanachama wa TCCIA pekee, hivyo kulifanya baraza hilo kutokuwa na uwakilishi wa sekta zingine kama jumuiya za wakulima, wafugaji, wafanyabiashara wadogo, bodaboda, baba lishe na mama lishe, wachimba madini, wabeba mizigo, wafugaji nyuki, wasindika unga na mafuta, wafanyabiashara wakubwa, wamiliki wa vyombo vya usafiri, wamiliki wa mabucha na wachoma nyama, bodi ya soko la Kibaigwa na taasisi za fedha.
Katika Mkutano wa uzinduzi upya wa Baraza, Mwenyeki wa Barza ambaye ni Mkuu wa Wilaya alitaka Baraza hili jipya kuwa lenye tija kwa kutimiza maazimio yote yaliyopitishwa kuendana na muda, hivyo kuifanya Kongwa ikue katika sekta ya biashara na uwekezaji na hatimaye kuongeza mapato ya Halmashauri na kuboresha uchumi wa wananchi wa Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.