Jumla ya miche ya miti 300,000 yazalishwa tayari kwa ajili ya kupandwa katika msimu huu wa mvua Wilayani Kongwa. Miche hiyo ya miti imeoteshwa katika vitalu vilivyopo maeneo tofauti-tofauti, ili kuwezesha kurahisihs a zoezi la usambazi kwa wananchi.
Afisa Kilimimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya (DAICO), Ndugu Jackson Shija ameeleza kwamba zoei la ugawaji miti limeshaanza ambapo miche 25,000 iliyokuwa katika kitalu cha Ibwaga - Kikundi cha Uzima imeanza kugawiwa kwa wanachi tarehe 4 Januri, 2018.
Aidha, DAICO ameeleza kuwa miongoni mwa miche hiyo laki tatu; miche 23,000 ipo katika kitalu cha Ibwaga, miche 23,000 kitaulu cha Chamkoroma, miche 200,000 kitali cha Magereza Mkoka na miche 54,000 kitalu cha Mkoka-Mrisho. Vitalu hivyo vina miche ya miti tofautitofauti, lakini mingi miongi ni miche ya korosha ambayo itagawiwa bure kwa wakulima watakaoomba kuichukua.
Wakulima watagawiwa kulingana na ukubwa wa shamba, hivyo wananchi na taasisi mbalimbali wanahimizwa kufika katika maeneo ya vitalu tajwa hapo juu kuchukua miche hiyo na kuipanda katika kipindi hiki cha msimu wa mvua kabla ya mvua za kwanza hazijaisha.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.