MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KONGWA WANOLEWA
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari – Kongwa DC
Afisa utumishi Wilaya ya Kongwa Bw. Fortunatus Mabula amewataka maafisa maendeleo ya jamii kuwajibika katika majukumu yao ya kazi hususani ufuatiliaji wa mikopo ya 10% kuhakikisha Wananchi wanajikwamua na umasikini.
Bw. Mabula ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi cha divisheni ya maendeleo ya jamii kilichofanyika Septemba 16 kikiwa na lengo la kujadili uundaji wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake, ufuatiliaji wa mikopo 10%, usajili wa vikundi, taarifa za utekelezaji wa mifumo ya IMES, PEPMIS, na kizazi chenye usawa na masuala ya msaada wa kisheria.
Pichani Afisa utumishi Wilaya ya Kongwa Bw. Fortunatus Mabula akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kongwa.
Vilevile Bw, Mabula licha ya kuwasihi maafisa maendeleo ya jamii kujiendeleza kielimu lakini pia amewasihi kulinda maadili ya kazi kuona namna bora ya kufanya kazi na jamii na kuheshimiana wao kwa wao.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakiwa katika kikao hicho.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kongwa Bi. Paskalina Duwe amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kila Kata kuwepo katika vituo vyao vya kazi na kuhudumia Wananchi muda wote, kujiepusha na makundi yasiyofaa na kuzingatia mambo yote muhimu yaliyojadiliwa katika kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kongwa Bi. Paskalina Duwe akiongea katika kikao hicho.
Nae Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) alipohudhuria kikao hicho ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa ushirikiano waliokuwa nao katika kipindi chote cha mpango wa Tasaf awamu ya tatu mpaka unapokwenda kuisha septemba 2025.
Mratibu wa Mpango wa kunusuru kaya masikini (Tasaf) Wilaya ya Kongwa Bw. Elias Chilemu akiongea katika kikao hicho.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.