Katika kuelekea kwenye uzinduzi wa matumizi ya mifumo mipya ya Mipango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (PlanRep) na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji wa Taarifa za Fedha Kwenye Vituo vya Kutolea Huduma (FFARS), mafunzo kwa watumiaji wa mfumo huo yanaendelea kutolewa kati hatua ya mwisho. Mafunzo haya yalitolewa kwa njia ya kanda na sasa yanaendelea kwa kanda ya Kati Mjiji Dodoma ambapo uzinduzi kitaifa utafanyika tarehe 5 Septemba 2017 na Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mfumo huu mpya wa Mpango na Bajeti kwa serikali za Mitaa utapatikana kwa njia ya mtandao tofauti na ilivyokuwa awali - mabadiliko ni kutoka kujitegemea (stand alone) na kuwa katika mfumo wa kitovuti (web based), pia, una maboresho kwa baadhi ya vipengele kulingana na maoni au mapendekezo yaliyotolewa na watumiaji toka kada mbalimbali. Mfumo huu umebuniwa na kutengenezwa na watanzania, kitu ambacho kinadhihirisha kwamba teknolojia imekuwa na Serikali ni wakati wa kuwaamini wataalam wa ndani katika kutatua changamoto mbalimbali kwa kutumia mifumo ya TEHAMA.
Mafunzo ya matumizi ya mifumo hii mipya ambayo itatumika mara tu baada ya uzinduzi; PlanRep ni kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 na mfumo wa FFARS utaanza kwa bajeti ya mwaka huu 2017/18. Mafunzo kwa sasa yanatolewa kwa Afisa Mipango (W), Afisa TEHAMA (W),Mweka Hazia (W), Mganga Mkuu na Katibu wa Afya ambao wanajukumu la kwenda kuwafundisha Maafisa wengine katika Idira na Vitengo zingine/vingine katika ngazi ya Halmashauri. Pia, mafunzo haya yanahusisha Maafisa toka ngazi ya Mkoa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.