Katibu Tawala Wilayani Kongwa Bw. Audiphace Mushi akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, amepiga marufuku Utupaji wa Taka ovyo, kwa Wananchi na wageni wapitao Katika eneo la Hifadhi ya Ranchi ya Taifa (NARCO) iliyopo wilayani humo na kuwa na desturi ya utunzaji wa Mazingira ili kuepuka uchafuzi holela wa Mazingira.
Akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo wa barabarani na wafanyakazi wa NARCO katika kituo cha mabasi cha Njia Panda ya Kiteto kilichopo eneo la NARCO katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani amesema, ni muhimu kufanyia usafi eneo hilo kila siku, na kuwa walinzi wa watupa taka wakiwemo abiria wa magari mbalimbali yanayosimama kwa ajili ya kununua bidhaa zao.
Aidha, amewataka Wananchi hao kutambua ya kuwa kuharibu Mazingira kunagharimu vizazi na vizazi, kutokana kutumia muda mrefu kutunza miti na uoto wa asili lakini katika kukata miti au kuchoma moto uoto wa asili hutumia sekunde chache.
Ambapo Sherehe hizo zilipambwa Kauli mbiu Kitaifa ilikuwa "Mkaa ni Gharama Tumia Nishati Mbadala"
Mushi alisema kimsingi vitendo vya Kibinadamu ndio Chanzo cha Uharibifu wa Mazingira, ikiwa ni pamoja na uchimbaji holela wa madini, ukataji miti ovyo, urinaji wa asali kwa kuchoma moto, uvamizi wa shughuli za kilimo maeneo ya milima.
Kadhalika alieleza kuwa, upo uchafuzi wa Taka ngumu eneo la Hifadhi ya NARCO, kama mifuko ya plastiki, makopo ya plastiki ambazo hutupwa na mabasi ya abiria na magari ya mizigo, pamoja na makondakta kutapisha vyombo vyao vya uchafu ndani ya Hifadhi. "Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya itakaa hivi karibuni na itatoa Tamko dhidi ya wachafuzi Mazingira NARCO", amesisitiza.
Meneja NARCO Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa alisema watamchulia hatua Kali za kisheria mtu yoyote watakaembaini anakata miti Katika Ranch hiyo bila kibali, pamoja na watakaovamia eneo hilo kwa ajili ya kilimo, na atakayechoma nyasi za moto kwenye eneo hilo, kwani ni malisho ya mifugo iliyopo katika Ranchi hiyo.
Aidha, ametoa ahadi ya kujenga choo katika kituo hicho ili kuepusha abiria wanachimbao dawa ovyo katika eneo hilo, na kuwataka vijana wafanyao biashara ndogondogo kujisajili na kutambulika na kuwa walinzi dhidi ya watupa taka na kukitunza na kukisimamia choo hicho.
Naye Kaimu Afisa Mazingira (W) Wilayani Kongwa, Bw. Godfrey Mujairi amesema kauli mbiu ya Mhe. Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Magufuli, inahamasisha Viwanda, hivyo viwanda haviwezi kuwepo kama uharibifu wa Mazingira, kwani malighafi na nishati, vyote hutokana na mazingira.
Mujairi ameongeza kuwa Utunzaji wa Mazingira usiishie siku ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Bali iwe ni Desturi yao Kila Siku kabla ya kufungua biashara.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.