Na Stephen Jackson, Kongwa.
Taasisi ya Tembea Kwa Matumaini Organization (TMO) imewasilisha rasimu ya ujenzi wa Kituo cha michezo kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Mbande Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa rasimu ya awali iliyowasilishwa Mei 15, 2023 na msanifu Fadhili Ally Namkumbe kutoka Place plan Consultant, ujenzi utagharimu takribani shilingi bil 12, na utahusisha viwanja mbalimbali ikiwemo mpira na riadha, na umekadiriwa kujazwa na mashabiki 7000.
Mkurugenzi Mtendaji Halmahauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary A. Nkullo kwa kushiirikiana na wakuu wa Divisheni na vitengo sanjali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, wameridhia mpango huo ingawa wamependekeza maboresho kwa baadhi ya miundombinu.
Kwa hatua hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo (TMO) Bwana Mohamed Hemed, ametoa shukrani za pekee kwa wajumbe wa kikao hicho cha kupitisha rasimu na ameahidi shughuli za ujenzi kuanza mara moja chini ya kampuni ya Salehe Contractors Ltd iliyojenga uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa viongozi wa taasisi hiyo ujenzi wa Kituo hicho cha michezo utaleta tija kwa wananchi wananchi kwani utahusisha maeneo ya vitega uchumi mbalimbali yakiwemo maduka na huduma nyinginezo.
Aidha bajeti ya ujenzi wa kituo hicho cha michezo, inatarajiwa kutatokana na michango ya wadau mbalimbali wa michezo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.