'Kutokana na mabadiliko ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (iCHF) ambapo Serikali imeamua huduma za Mfuko huu kutumika nchi nzima, kila kaya (Familia ya watu 6) italipa shilingi elfu thelathini (30,000/=)".
Hayo yamesemwa na Mhe White Zuberi Mwanzalila wakati akifungua mafunzo ya maafisa waandikishaji wa Mfuko huo kwa Wilaya ya Kongwa tarehe 9 JUlai, 2018. Aidha, ameeleza kwamba hatua za huduma za CHF kupanuliwa ni mpango wa serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake na lengo ni kila mwananchi kuwa na uhakika wa kupata matibu wakati wote.
Pia, amesema malipo mapya yataanza mara tu baada ya taratibu za vikao vya kisheria kukamila mwishoni mwa mwezi huu.
Katika Mafunzo hayo zaidi ya maafisa waandikshaji 100 pamoja na maafisa wasimamizi wa CHF Wilaya na Tarafa Wilayani Kongwa walipata Mafunzo ambayo yalifadhiliwa na wadau wa HPSS.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.